Wednesday, January 11, 2012

VYOO TUMAINI VYAWA KERO KWA WANAFUNZI




Vyoo katika chuo kikuuu cha tumaini maeneo ya mikocheni vimekuwa kero kubwa kwa wana funzi wanaosoma katika chuo hicho,wakizungumza kwa nyakati tofauti wabafunzi hao wamesema vyoo hivyo vimekuwa vikitoa harufu mbaya ambayo inaingia madarasani na kusababisha wanafunzi kupunguza usikivu kwa walimu wanapokuwa madarasani.

Vyoo hivyo mbali na kutoa harufu mbaya pia vipo katika mazingira ya usafi ambayo hairidhishi
kwani ni vichafu na hakuna maji kwa ajili ya kutumia chooni hivyo kusababisha kuwa katika hali mbaya ya hiyo ya uchafu.

Wakizungumzia kuhusu tatizo hilo wafanyakazi wanaofanya usafi  katika chuo hicho wamesema  hali hiyo ambayo ni ya muda mrefu sasa inasababishwa na tatizo la la upungufu wa maji uliopo chuoni hapo .

 

agnesshija2005@yahoo.com




No comments:

Post a Comment